Kumbukizi ya Kwanza ya Falsafa ya ‘Hapa Kazi Tu’
Richard Mbunda
Richard Mbunda
Siku hizi tumetumbukia kwenye mtego wa mipango ya muda mfupi ndio maana tunajikita kutathmini hata siku 100 tu za Rais mpya madarakani! Wanazuoni wanasema utaratibu huu ulianza tangu enzi za Napoleoni, lakini ulitamalaki zaidi kuanzia wakati wa Rais Franklin Roosevelt wa Marekani mwaka 1933 hata sasa. Japo siku 100 zinaweza kutupa mwelekeo wa viongozi na falsafa zao, walakini kipimo sahihi cha kiongozi mpya si budi kiwe mwaka mmoja na sio miezi kadhaa tu kwa kuzingatia uzito wa kazi yenyewe. NIONYE juu ya mipango ya muda mfupi kwani inatufanya tusahau ya muda mrefu. Kwa mfano, kuna barabara zinadumu mwaka mmoja tu kisha tunarudia tena ujenzi kitu ambacho kinatunyima uwekezaji wenye tija maeneo mengine. Vivyo hivyo, tunakosa kufanya uwekezaji wa muda mrefu katika rasilimali watu n.k.
Mwaka mmoja wa Ofisi Kuu kwa Mkuu wa Kaya uliadhimishwa sambamba na siku yake ya kuzaliwa. Hata hivyo kuna gazeti moja limeandika kuwa majukumu yalimfanya Mkuu wa Kaya asahau siku yake ya kuzaliwa. Hii inatuonyesha ni jinsi gani Tanzania ilivyo akilini mwa Mkuu wa Kaya kuliko kumbukumbu ya kuzaliwa kwake. Nadhani pia ameanza kuwapa uhalisia wa mambo wale waliokuwa wanakesha kuifikiria Ikulu wakidhani ni pahala pa kugonga cheers tu! Naam, ilitushangaza kidogo pale ambapo kila mtu tu alidhani anaweza kuvaa viatu vya ukuu wa kaya. Naamini mpaka aje atoke madarakani watu watajiuliza mara mbilimbili kama haswaaa wanaweza kuvaa viatu vyake.![]()
Mkuu wa Kaya, umetimiza mwaka mmoja ofisini katika ngazi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi. Leo sitazungumzia hatua yako ya kuzuia shughuli za kisiasa bila sababu ya msingi, au ile hotuba yako iliyoleta mtafaruku kule Zanzibar, bali nikiri tu kuwa katika kipindi chako cha mwaka mmoja kila Mtanzania hata wapinzani wako kwa namna moja au nyingine wameridhika na utendaji wako. Wino umemwagwa vya kutosha kuelezea mafanikio yako ndani na nje ya mipaka yetu. Umeleta heshima ya kazi katika utumishi wa umma na umekuwa mfano wa kuigwa katika utendaji kazi. Pia umewafanya wafanyakazi wa kawaida kujawa na hisia za uzalendo na moyo wa kuitumikia nchi yao.
Umeleta pia mabadiliko katika matumizi ya mali ya umma. Mimi huwa napingana na wale wanaosema unabana matumizi, si kweli bali umeondoa matumizi mabaya. Matumizi ya bilioni mbili kusherehekea siku ya uhuru ni matumizi mabaya ya pesa za umma. Kutenga bilioni mbili kwa ajili ya semina elekezi kwa mawaziri ni matumizi mabaya ya pesa za umma. Kusafirisha viongozi wote wa kitaifa wakahudhuria kuzimwa kwa Mwenge wa Uhuru ni matumizi mabaya ya rasilimali watu na pesa za umma. Hatua nzuri ulizichukua na Tanzania ikapongeza. Lakini naomba usiishie hapo. Maana ukiondoka kesho matumizi haya yasiyo na tija yanaweza kurudishwa na watu wasio na nia njema na Tanzania huko mbeleni. Ni muda muafaka sasa mambo haya tuyawekee KANUNI za kuyazuia. Ukiamua linawezekana.![]()
Mheshimiwa Mkuu wa Kaya, wafanyakazi hewa, wanafunzi hewa na miradi hewa umeishughulikia kwa umahiri mkubwa. Vita hii uliyoianzisha imekuwa muhimu sana kwani taifa limepoteza pesa mingi katika ghiliba hizi za ‘mabosi’ wa vitengo vya umma. Hili nalo tuliundie mfumo. Wakishasafisha hao wachafuzi na majizi ya pesa za umma itatupasa sasa tuwe na kanzidata (database) moja itakayomulika wafanyakazi wote na taarifa zao za kuachishwa kazi au vifo.
Mkuu wa Kaya, jitihada zako kuhusu kupambana na rushwa na uporwaji wa mali ya umma ni wa kupongezwa sana. Umeacha gumzo kila kona kwa jinsi ulivyobana mianya na zile njia za panya… kwa wale walioiona nchi hii kama shamba la bibi. Kusema kweli huku mtaani hali si hali. Lakini ni ukweli usiofichika tulizoea kuishi kiujanja ujanja! Hatuna budi kuisoma namba. Hatua yako ya kuanzishwa mahakama ya majizi na mafisadi itakuwa ya mfano kwa Afrika, na naamini Afrika na sio Tanzania pekee itakukumbuka kwa hatua hii.
Mkuu wa Kaya, watu sasa wanalipa kodi, na watu wanadai risiti. Lakini, niruhusu nikunong’oneze kidogo katika hili. Kuna mapungufu kadhaa kwenye kale kamashine ka kutolea risiti (EFD) kwani hakana maelezo (description) ya bidhaa ulizochukua, bali kanatoa jumla tu. Na hawa ndugu wafanyabishara wamegundua mtindo wa kupunguza tarakimu moja tu, lakini madhara yake unayajua. Kwa mfano, badala ya kutoa risiti ya shilingi 500,000 watatoa risiti ya shilingi 50,000.![]()
Mkuu wa Kaya, mimi binafsi nimefurahishwa na teuzi zako, hasa wa Msaidizi wako Mkuu yule Waingereza wanamuita Premier. Natambua ya kuwa, kipimo cha kwanza cha kiongozi ni namna anavyopanga safu yake ya wasaidizi. Kinachonifurahisha zaidi ni jinsi ulivyowapoteza maboya watu katika uteuzi wako. Wengi hawakumdhania, lakini Premier amekuwa nguzo imara katika utawala wako. Kwa kuzingatia hulka, mawasiliano yake kwa umma, na utekelezaji wa majukumu yake huyu Premier ni mfano wa kuigwa. Amekuwa chachu ya utekelezaji wa kaulimbiu ya "Hapa Kazi Tu", lakini pia anaheshimika kwa umma wa Watanzania. Ukitaka ushahidi nitakupatia…... nikunong’oneze tu, Premier ni kiongozi pekee ambaye hatajwi kwa mizaha au kejeli katika mitandao ya kijamii hasa kuleee unakokujua.
NI MWAKA MMOJA SASA: Mheshimiwa Mkuu wa Kaya, katika utekelezaji wa ilani yako ya uchaguzi mimi nakunwa sana na mipango ya ujenzi wa reli ‘standard gauge’. Mimi naamini reli itachangamsha sana uchumi wetu hasa kama Dodoma unakohamishia makao yako utaifanya kuwa HUB ikaunganishwa na reli kwenda Pwani, Kanda ya Ziwa, Kusini, Rukwa mpaka Kigoma. Kama nchi tumekuwa na utegemezi wa hali ya juu wa barabara kusafirisha abiria na mizigo. Ndio maana ajali zinaongezeka kila leo na kwa kiasi kikubwa uchumi wetu unaathiriwa. Wakulima kule kijijini wamekosa faida katika mazao yao kwa kuwa miundombinu ya usafirishaji ni mibovu, na japo mazao yao yanahitajika kwa wingi sehemu zinginezo lakini wanakatishwa tamaa na suala la usafirishaji. Mkuu wa Kaya, naamini utaitumikia nchi hii miaka 10. Hivyo basi, ujenzi wa reli, ambao naamini ni gharama kubwa, na uwe nembo ya utawala wako uliotukuka.![]()
Mipango yako ya mabadiliko nilipenda pia imulike jambo hili linalohusu SHERIA. Mkuu wa Kaya, Bunge letu linapanuka kila mwaka. Kwa Mamlaka ya NEC na ZEC kule Zanzibar kila baada ya miaka kadhaa wanafanya mapitio na kuona ni jinsi gani wabadili mipaka ya majimbo kitu ambacho kimekuwa kikiongeza idadi ya majimbo. Mkuu wa Kaya utakubaliana na mimi kuwa hatuhitaji wabunge 500 kulifanya bunge liwe wakilishi au lifanye kazi yake ya kutunga sheria na kuisimamia serikali kwa ufasaha! Na tukitaka uwakilishi kwa idadi ya watu basi China na India zingekuwa wa wabunge walao elfu kumi. Huku ni kuongeza gharama na ugumu wa maisha ya mtanzania wa kawaida bila sababu. Mkuu wa Kaya, unaweza kutukomboa katika mwelekeo huu. Tunapaswa kuweka STOP uongezwaji wa majimbo ya Ubunge na viti maalumu. Mimi nilipenda sana pendekezo la Tume ya Jaji Warioba, iliyopendekeza kila Mkoa wa Tanzania Bara na Wilaya za Zanzibar kutoa wabunge wawili, wa kike na wa kiume, na Rais wa Jamhuri achague wabunge watano tu. Kwa mfano, hakuna sababu ya eneo la watu milioni moja na laki mbili tu kama Zanzibar wawe na majimbo 54 ya uwakilishi na 50 ya Ubunge kama ilivyokuwa 2015. Hatuwezi kupiga hatua za kimaendeleo kama tuna kada kubwa ya viongozi wanaoongeza matumizi kuliko uwekezaji.
Mwaka mmoja wa Ofisi Kuu kwa Mkuu wa Kaya uliadhimishwa sambamba na siku yake ya kuzaliwa. Hata hivyo kuna gazeti moja limeandika kuwa majukumu yalimfanya Mkuu wa Kaya asahau siku yake ya kuzaliwa. Hii inatuonyesha ni jinsi gani Tanzania ilivyo akilini mwa Mkuu wa Kaya kuliko kumbukumbu ya kuzaliwa kwake. Nadhani pia ameanza kuwapa uhalisia wa mambo wale waliokuwa wanakesha kuifikiria Ikulu wakidhani ni pahala pa kugonga cheers tu! Naam, ilitushangaza kidogo pale ambapo kila mtu tu alidhani anaweza kuvaa viatu vya ukuu wa kaya. Naamini mpaka aje atoke madarakani watu watajiuliza mara mbilimbili kama haswaaa wanaweza kuvaa viatu vyake.

Mkuu wa Kaya, umetimiza mwaka mmoja ofisini katika ngazi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi. Leo sitazungumzia hatua yako ya kuzuia shughuli za kisiasa bila sababu ya msingi, au ile hotuba yako iliyoleta mtafaruku kule Zanzibar, bali nikiri tu kuwa katika kipindi chako cha mwaka mmoja kila Mtanzania hata wapinzani wako kwa namna moja au nyingine wameridhika na utendaji wako. Wino umemwagwa vya kutosha kuelezea mafanikio yako ndani na nje ya mipaka yetu. Umeleta heshima ya kazi katika utumishi wa umma na umekuwa mfano wa kuigwa katika utendaji kazi. Pia umewafanya wafanyakazi wa kawaida kujawa na hisia za uzalendo na moyo wa kuitumikia nchi yao.
Umeleta pia mabadiliko katika matumizi ya mali ya umma. Mimi huwa napingana na wale wanaosema unabana matumizi, si kweli bali umeondoa matumizi mabaya. Matumizi ya bilioni mbili kusherehekea siku ya uhuru ni matumizi mabaya ya pesa za umma. Kutenga bilioni mbili kwa ajili ya semina elekezi kwa mawaziri ni matumizi mabaya ya pesa za umma. Kusafirisha viongozi wote wa kitaifa wakahudhuria kuzimwa kwa Mwenge wa Uhuru ni matumizi mabaya ya rasilimali watu na pesa za umma. Hatua nzuri ulizichukua na Tanzania ikapongeza. Lakini naomba usiishie hapo. Maana ukiondoka kesho matumizi haya yasiyo na tija yanaweza kurudishwa na watu wasio na nia njema na Tanzania huko mbeleni. Ni muda muafaka sasa mambo haya tuyawekee KANUNI za kuyazuia. Ukiamua linawezekana.

Mheshimiwa Mkuu wa Kaya, wafanyakazi hewa, wanafunzi hewa na miradi hewa umeishughulikia kwa umahiri mkubwa. Vita hii uliyoianzisha imekuwa muhimu sana kwani taifa limepoteza pesa mingi katika ghiliba hizi za ‘mabosi’ wa vitengo vya umma. Hili nalo tuliundie mfumo. Wakishasafisha hao wachafuzi na majizi ya pesa za umma itatupasa sasa tuwe na kanzidata (database) moja itakayomulika wafanyakazi wote na taarifa zao za kuachishwa kazi au vifo.
Mkuu wa Kaya, jitihada zako kuhusu kupambana na rushwa na uporwaji wa mali ya umma ni wa kupongezwa sana. Umeacha gumzo kila kona kwa jinsi ulivyobana mianya na zile njia za panya… kwa wale walioiona nchi hii kama shamba la bibi. Kusema kweli huku mtaani hali si hali. Lakini ni ukweli usiofichika tulizoea kuishi kiujanja ujanja! Hatuna budi kuisoma namba. Hatua yako ya kuanzishwa mahakama ya majizi na mafisadi itakuwa ya mfano kwa Afrika, na naamini Afrika na sio Tanzania pekee itakukumbuka kwa hatua hii.
Mkuu wa Kaya, watu sasa wanalipa kodi, na watu wanadai risiti. Lakini, niruhusu nikunong’oneze kidogo katika hili. Kuna mapungufu kadhaa kwenye kale kamashine ka kutolea risiti (EFD) kwani hakana maelezo (description) ya bidhaa ulizochukua, bali kanatoa jumla tu. Na hawa ndugu wafanyabishara wamegundua mtindo wa kupunguza tarakimu moja tu, lakini madhara yake unayajua. Kwa mfano, badala ya kutoa risiti ya shilingi 500,000 watatoa risiti ya shilingi 50,000.

Mkuu wa Kaya, mimi binafsi nimefurahishwa na teuzi zako, hasa wa Msaidizi wako Mkuu yule Waingereza wanamuita Premier. Natambua ya kuwa, kipimo cha kwanza cha kiongozi ni namna anavyopanga safu yake ya wasaidizi. Kinachonifurahisha zaidi ni jinsi ulivyowapoteza maboya watu katika uteuzi wako. Wengi hawakumdhania, lakini Premier amekuwa nguzo imara katika utawala wako. Kwa kuzingatia hulka, mawasiliano yake kwa umma, na utekelezaji wa majukumu yake huyu Premier ni mfano wa kuigwa. Amekuwa chachu ya utekelezaji wa kaulimbiu ya "Hapa Kazi Tu", lakini pia anaheshimika kwa umma wa Watanzania. Ukitaka ushahidi nitakupatia…... nikunong’oneze tu, Premier ni kiongozi pekee ambaye hatajwi kwa mizaha au kejeli katika mitandao ya kijamii hasa kuleee unakokujua.
NI MWAKA MMOJA SASA: Mheshimiwa Mkuu wa Kaya, katika utekelezaji wa ilani yako ya uchaguzi mimi nakunwa sana na mipango ya ujenzi wa reli ‘standard gauge’. Mimi naamini reli itachangamsha sana uchumi wetu hasa kama Dodoma unakohamishia makao yako utaifanya kuwa HUB ikaunganishwa na reli kwenda Pwani, Kanda ya Ziwa, Kusini, Rukwa mpaka Kigoma. Kama nchi tumekuwa na utegemezi wa hali ya juu wa barabara kusafirisha abiria na mizigo. Ndio maana ajali zinaongezeka kila leo na kwa kiasi kikubwa uchumi wetu unaathiriwa. Wakulima kule kijijini wamekosa faida katika mazao yao kwa kuwa miundombinu ya usafirishaji ni mibovu, na japo mazao yao yanahitajika kwa wingi sehemu zinginezo lakini wanakatishwa tamaa na suala la usafirishaji. Mkuu wa Kaya, naamini utaitumikia nchi hii miaka 10. Hivyo basi, ujenzi wa reli, ambao naamini ni gharama kubwa, na uwe nembo ya utawala wako uliotukuka.

Mipango yako ya mabadiliko nilipenda pia imulike jambo hili linalohusu SHERIA. Mkuu wa Kaya, Bunge letu linapanuka kila mwaka. Kwa Mamlaka ya NEC na ZEC kule Zanzibar kila baada ya miaka kadhaa wanafanya mapitio na kuona ni jinsi gani wabadili mipaka ya majimbo kitu ambacho kimekuwa kikiongeza idadi ya majimbo. Mkuu wa Kaya utakubaliana na mimi kuwa hatuhitaji wabunge 500 kulifanya bunge liwe wakilishi au lifanye kazi yake ya kutunga sheria na kuisimamia serikali kwa ufasaha! Na tukitaka uwakilishi kwa idadi ya watu basi China na India zingekuwa wa wabunge walao elfu kumi. Huku ni kuongeza gharama na ugumu wa maisha ya mtanzania wa kawaida bila sababu. Mkuu wa Kaya, unaweza kutukomboa katika mwelekeo huu. Tunapaswa kuweka STOP uongezwaji wa majimbo ya Ubunge na viti maalumu. Mimi nilipenda sana pendekezo la Tume ya Jaji Warioba, iliyopendekeza kila Mkoa wa Tanzania Bara na Wilaya za Zanzibar kutoa wabunge wawili, wa kike na wa kiume, na Rais wa Jamhuri achague wabunge watano tu. Kwa mfano, hakuna sababu ya eneo la watu milioni moja na laki mbili tu kama Zanzibar wawe na majimbo 54 ya uwakilishi na 50 ya Ubunge kama ilivyokuwa 2015. Hatuwezi kupiga hatua za kimaendeleo kama tuna kada kubwa ya viongozi wanaoongeza matumizi kuliko uwekezaji.
MICHEZO: Mkuu wa Kaya, Watanzania wanapenda michezo. Utaliona hili siku Timu ya Taifa ikicheza mechi na timu kubwa au hata Yanga na Simba wanapokutana. Naamini pia unapenda michezo si ndio maana ukaomba kwa Mfalme wa Morocco uwanja mkubwa ujengwe Dodoma? Sisi ni nchi ya watu wanaokaribia miloni 50 lakini hatujajiendeleza kimichezo. Mzee Mwinyi alishawahi kutuita kichwa cha mwendawazimu… tumeendelea kuwa hivyo. Wakati wa michuano ya Olympic tulikuwa na wawakilishi wachache na aliyefahamika zaidi ni mwanariadha. Japo hakuleta medali lakini watanzania tulilipuka kwa furaha ya uwakilishi wake. Tuwekeze katika elimu ya michezo kama mkakati wa Serikali. Tujenge Vituo vya Michezo kwa kuanzia angalau katika kila kanda. Vituo hivi vihusishe michezo yote kuanzia mpira wa miguu, netball, bwawa la kuogelea, tennis, basketball, netball na cricket. Tunaweza kutumia vituo hivi kulea vipaji katika umri wa miaka 14 na kuendelea na tukapata professionals katika michezo mbalimbali. Vituo hivi vya michezo vikijengwa karibu na shule zilizopo vijana hawa watahudhuria madarasa ya kawaida na baadae kushiriki katika programu zao za michezo wakiwa hosteli maalum za vituo hivyo. Huu ni uwekezaji kwa kuwa vijana hawa wakiiva wataiingizia nchi mapato makubwa sana. Siamini pia kama gharama itakuwa kubwa zaidi. Tunayo mifano mizuri ya akina Mbwana Samatta, tunahitaji kutengeneza kama 1000 wengine achilia mbali watakaocheza hapa nchini. Ivory Coast ina wachezaji karibia kila nchi duniani ikiwemo Israel na hapa Tanzania, kwa nini sisi hatuna huko professionals huko nje?

Happy Birthday Mkuu wa Kaya!